Jumatano 25 Machi 2026 - 21:42
Spika wa Bunge la Uturuki Amekosoa Vikali Baadhi ya Watu Wanao Fungamana na Maslahi ya Marekani na Israel

Hawza/ Mustafa Şentop, Spika wa Bunge la Uturuki, katika hotuba yake amesisitiza juu ya nafasi na misimamo ya kisiasa kama kipimo cha kutathmini uzalendo wa watu, na amekosoa mwelekeo wa baadhi ya makundi kufuata maslahi ya nchi za kigeni.

Kwa mujibu wa Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Spika wa Bunge la Uturuki, Mustafa Şentop, katika ukurasa wake wa X, amewakosoa wale wanaofuatilia maslahi ya Marekani na Israel. Maandishi ya kauli yake ni kama ifuatavyo:

Katika kupima “kuwa wa kitaifa” kwa mtu yeyote, nafasi anayosimama ndiyo kigezo kikuu. Ikiwa dira yenu kila mara inaelekezwa kwenye Ikulu ya White House na maslahi ya Israel, basi hamtastahili tena kutoa kauli ya kweli kuhusu ardhi hizi [nchi za eneo hili].

Katika vita vinavyoendelea sasa imekuwa wazi kwa wote kwamba nyuma ya chuki dhidi ya Iran na upendeleo kwa Marekani na Israel kuna mtazamo “ulioagizwa.” Taifa hili lenye ufahamu linajua vyema ni kina nani wanaohusiana na kushirikiana na nani, na katika barabara ngapi za giza wanapita.

Spika wa Bunge la Uturuki Amekosoa Vikali Baadhi ya Watu Wanao Fungamana na Maslahi ya Marekani na Israel

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha